• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  KIEMBA, CHANONGO KUPELEKWA SIMBA B, KISIGA AWEZA KUSAMEHEWA BAADA YA KUOMBA RADHI

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inafikiria kuwapeleka timu ya pili, wachezaji wake wawili iliyowasimamisha viungo Amri Kiemba na Haroun Chanongo, wakati Shaaban Kisiga anaweza kusamehewa na kurejeshwa kikosi cha kwanza.
  BIN ZUBEIRY inafahamu Kisiga maarufu kama Malone kwa jina la utani ameomba msamaha kwa uongozi wa klabu hiyo, wakati Kiemba ‘Jeshi la Jiwe’ na Chanongo wao walijibu ‘jeuri’.
  Wote Kiemba na Chanongo walisema wako tayari kwa maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na uongozi wa klabu hiyo na kauli hiyo iliwakera viongozi wa Simba chini ya rais, Evans Aveva.
  Amri Kiemba atapelekwa Simba B akamalizie Mkataba wake

  Hatua ambayo sasa Simba wanataka kuichukua wakati wachezaji hao wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu ni kuwapeleka timu ya vijana chini ya kocha Nico Kiondo.
  Tayari Azam FC wamekwishawasilisha ombi Simba SC wakisema wanamtaka Kiemba, ingawa Wekundu wa Msimbazi bado hawajatoa jibu rasmi japo habari za ndani zinasema waliomba Sh. Milioni 15.
  Na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wanaona kwamba Sh Milioni 15 ni nyingi ikiwa mchezaji huyo wa zamani wa Yanga SC, Kagera Sugar, Miembani na Moro United anamaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu.
  Wachezaji hao wote watatu walisimamishwa Oktoba mwaka huu kwa tuhuma tofauti, Kiemba na Chanongo wakituhumiwa kucheza kwa kiwango cha chini, wakati Kisiga alidaiwa kuwajibu jeuri viongozi.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIEMBA, CHANONGO KUPELEKWA SIMBA B, KISIGA AWEZA KUSAMEHEWA BAADA YA KUOMBA RADHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top