• HABARI MPYA

  Wednesday, November 26, 2014

  KARIM NDUNGWA APIGA HAT TRICK VILLA IKISHINDA 4-0 UGANDA

  Karim Ndungwa ameipigia hat trick Villa jana
  MABAO matatu ya Karim Ndugwa yamechangia ushndi wa 4-0 kwa SC Villa dhidi ya Entebbe jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uganda Uwanja wa Nakivbo.
  Erisa Ssekisambu aliyetokea benchi alifunga bao la nne akirejea uwanjani kwa mara ya kwanza kufuatia kusimamishwa mwezi mmoja kwa utovu wa nidhamu.
  Ndugwa sasa anafikisha mabao saba anayomzidi Robert Ssentongo, na hiyo inakuwa hat-trick ya pili msimu huu.
  Matokeo hayo yanaifanya Villa iendelee kuwa nafasi ya pili kwa pointi zake 22, moja nyuma ya vinara, Vipers. Wapinzani wa Villa, Entebbe wanabaki nafasi ya tatu kutoka mkiani kwa pointi zao sita.
  Katika mechi nyingine za jana, bao pekee la Joshua Masene liliipa ushindi wa 1-0 Bul dhidi ya waburuza mkia Rwenshama Uwanja wa Kakindu, Jinja wakati Lweza na Bright Stars zilitoka sare ya 1-1 huko Wankulukuku.
  Fred Kalanzi aliifungia Lweza wakati Anthony Bongole akawafungia wageni huku Fred Kajoba ikifikisha mechi tatu bila kushinda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KARIM NDUNGWA APIGA HAT TRICK VILLA IKISHINDA 4-0 UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top