• HABARI MPYA

  Sunday, November 30, 2014

  HANS POPPE AREJEA KUTOKA ULAYA NA KUSEMA’ “USAJILI DIRISHA DOGO SAFI KABISA”

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amerejea usiku huu kutoka Ujerumani alipokuwa kwa mapumziko na amesema kila kitu kinaenda vizuri kuhusu usajili wa dirisha dogo.
  “Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati, nilipoondoka wana Kamati wengine walikuwepo na walikuwa wanaendelea kufanyia kazi maazimio, na kwa taarifa nilizonazo, kila kitu kinakwenda vizuri,”amesema Poppe akizungumza na BIN ZUBEIRY mida hii.
  Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba kocha Patrick Phiri alitoa mapendekezo yake juu ya wachezaji wa kusajili na yamefanyiwa kazi vizuri.
  Hans Poppe amerejea usiku huu kutoka Ujerumani

  “Nadhani baada ya siku mbili tatu hizi, wapenzi wa Simba SC watarajie kusikia habari nzuri, kila kitu kinakwenda safi kabisa,”amesema.
  Miongoni mwa wachezaji ambao wapo mawindoni Simba SC ni mfungaji bora wa Kenya kwa misimu miwili iliyopita, Mganda Dan Sserunkuma ambaye alikuwapo nchini siku nne zilizopita.
  Inadaiwa baada ya mazungumzo na maafikiano, Sserunkuma anayechezea Gor Mahia ya Kenya kwa sasa alirejea Uganda mara moja na wakati wowote atarudi Dar es Salaam kusaini Mkataba. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE AREJEA KUTOKA ULAYA NA KUSEMA’ “USAJILI DIRISHA DOGO SAFI KABISA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top