• HABARI MPYA

  Thursday, November 27, 2014

  BILEKU MPASI AJA KUTUMBUIZA DAR DESEMBA 12

  Na Samira, Said, DAR ES SALAAM
  MWANAMUZIKI mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Bileku Mpasi, anatarajiwa kuja nchini kusindikiza utambulisho wa nyimbo mbili mpya za bendi ya Mashujaa utakaofanyika Desemba 12 mwaka huu kwenye ukumbi wa Ten Lounge.
  Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, mratibu wa onyesho hilo, King Dodoo, alisema kuwa Mpasi ambaye alitamba katika tasnia ya muziki wa dansi alipokuwa na gwiji, marehemu, Pepe Kale, atakuja na wasanii wengine ili kutoa burudani ya kiwango cha juu.
  Dodoo alitaja nyimbo hizo mbili ambazo zitatambulishwa ni pamoja na Rafiki Sokoni na My Queen.

  Rais wa bendi ya Mashujaa Chalz Baba, akizungumzia utambulsiho wa nyimbo zao mbili ambao utafanyika Disemba 12 mwaka huuu, kwenye Ukumbi wa Ten Lounge, utasindikizwa na mwanamuziki Bileku Mpasi kutoka nchini Congo, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Mashujaa Group, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Mabibo Bear, ambao wamedhamini onesho hilo.

  Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi nchini kujiandaa kushuhudia onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria hapa nchini.
  Rais wa Mashujaa Musica, Chalz Baba, alisema kuwa wamejiandaa kutoa burudani nzuri na kuendeleza heshima yao ya bendi bora kwa mwaka wa pili mfululizo.
  " Napenda kuwahakikishia wapenzi wa bendi yetu tutafanya kazi ya ubora wa juu, ni kawaida yetu kufanya kazi nzuri, tuna usongo," alisema Chalz.
  Nawe mwakilishi wa Windhoek ambao ni wadhamini wa onyesho hilo, Joseph Emmanuel, alisema wameamua kudhamini utambulisho huo ili kuendeleza muziki wa dansi nchini kufikia hadhi ya kimataifa.
  Mashujaa pia itatumbuiza nyimbo zake zilizotamba katika albamu zake za Risasi Kidole na Ushamba Mzigo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BILEKU MPASI AJA KUTUMBUIZA DAR DESEMBA 12 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top