• HABARI MPYA

  Tuesday, November 25, 2014

  KOCHA HARAMBEE STARS KUTUA AFC

  Amrouche kushoto akiwa na kocha
  wa zamani wa Tanzania, Mdenmark Kim Poulsen
  TIMU ya AFC Leopards ya Ligi Kuu ya Kenya ipo kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Adel Amrouche ili Mualgeria huyo achukue nafasi ya Pieter De Jongh ambaye ameitema klabu hiyo.
  Chanzo cha habari kimesema kwamba mazungumzo baina ya panda hizo mbili yanaendelea vizuri na kwamba Amrouche anaweza kutambulishwa wakati wowote tayari kuanza kazi kwa ajili ya msimu wa 2015 wa KPL.
  De Jongh alichukua nafasi ya James Nandwa aliyefukuzwa katikati ya msimu wa 2014 baada ya kuiongoza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya sita kwenye ligi.
  Hata hivyo, kiwango cha timu chini ya kocha huyo Mholanzi hakikuuvutia uongozi wa Leopards na ukawa mwanzo wa kuelekea mlango wa kutokea.
  Amrouche alikuwa kocha wa Harambee Stars kuanzia mwaka 2013, lakini akafukuzwa na Shirikisho la Soka Kenya baada ya kushindwa kufuzu kwenye fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015. 
  Mshindi wa Kombe la CECAFA Challenge mwaka jana akiwa na Harambee Stars, awali, alifundisha timu za Burundi na Equatorial Guinea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA HARAMBEE STARS KUTUA AFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top