• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  TFF YATOA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNYUKU, KARASHANI

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko vifo vya waandishi wa habari Innocent Munyuku na Baraka Karashani vilivyotokea jana (Novemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
  Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu, na tasnia ya habari nchini kwa ujumla kutokana na mchango mkubwa waliotoa katika ustawi wa mpira wa miguu nchini kupitia kalamu zao.
  Baraka Karashani kushoto na Innocent Munyuku kulia enzi za uhao wao

  Munyuku alikuwa mmoja wa waandishi waanzilishi wa gazeti la Mwanaspoti wakati Karashani kwa nyakati tofauti alifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo kampuni ya New Habari 2006 akiripoti habari za mpira wa miguu.
  Tunatoa pole kwa familia za marehemu, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), na kampuni ya New Habari 2006 na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YATOA RAMBIRAMBI MSIBA WA MUNYUKU, KARASHANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top