• HABARI MPYA

  Monday, November 24, 2014

  KIEMBA AANZA KAZI RASMI AZAM FC

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Amri Kiemba, leo ameanza mazoezi na klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Azam FC maana yake mpango wa kuhamia Chamazi umefanikiwa.
  Azam FC iliwasilisha barua rasmi Simba SC ya kumuomba kiungo Kiemba, ambaye kwa sasa yupo kwenye matatizo na klabu yake. 
  Amri Kiemba anatakiwa Azam FC
  Mwishoni mwa mwezi uliopita, Kiemba pamoja na viungo wengine wa klabu hiyo, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Haroun Chanongo walisimamishwa Simba SC kwa sababu tofauti. 
  Wakati Kiemba na Chanongo walidaiwa kucheza chini ya kiwango chao tofauti na wanavyokuwa timu ya taifa, Taifa Stars- Kisiga alidaiwa kuwatolea majibu ya kifedhuli viongozi.
  Wachezaji hao walipatwa na mkasa huo baada ya timu kulazimishwa sare ya tano mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1-1 na Prisons mjini Mbeya.
  Baada ya kusimamishwa kwao, Simba SC ilitoa sare tena na Mtibwa Sugar mjini Morogoro kabla ya kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting 1-0 mjini Dar es Salaam.

  Wakati Kiemba aliyewahi kuchezea pia Yanga SC, Moro United, Miembeni na Kagera Sugar anakwenda Azam FC, Chanongo atapelekwa timu B na Kisiga anaweza kusamehewa baada ya kuomba radhi kwa uongozi. 
  Amri Kiemba akiwa mazoezini Azam FC leo asubuhi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIEMBA AANZA KAZI RASMI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top