• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  MASHINDANO YA TAIFA YA U12 YASOGEZWA

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  MASHINDANO ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yanayoshirikisha kombaini za mikoa yote ya Tanzania yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 30 mwaka huu hadi Januari 5 mwakani.
  Awali mashindano hayo yalipangwa kuanza Desemba 6 mwaka huu, lakini yamelazimika kuyasogeza ili kutoa fursa ya kukamilika kwa matengenezo ya viwanja vitatu ambayo vitatumika.
  Kila timu ya mkoa inatakiwa kuwa na ujumbe wa watu 16, wakiwemo wachezaji 14 na makocha wawili katika mashindano hayo ya timu yenye wachezaji saba (7 aside).
  Mashindano hayo yanalenga kuunda timu imara ya vijana chini ya umri wa miaka 17

  Timu zinatakiwa kuwasili jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu tayari kwa ajili ya uhakiki wa umri na taratibu nyingine za mashindano. Timu zote zitafikia katika shule ya Alliance (Alliance Schools).
  Wachezaji wanaotakiwa kushiriki mashindano hayo ni wenye umri chini ya miaka 12, hivyo ni wale waliozaliwa kuanzia Januari 2003 na kuendelea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHINDANO YA TAIFA YA U12 YASOGEZWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top