• HABARI MPYA

  Friday, November 28, 2014

  TRAORE ANASA RADA ZA YANGA SC, MAXIMO AWAAMBIA VIONGOZI; “NILETEENI KIFAA HICHO HARAKA”

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAWAZO ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo yamegongana na ya viongozi wa Yanga SC, wote wanamtaka mshambuliaji wa Mali, Mohamed Traore.
  Wakati Maximo akiwa likizo Brazil, viongozi wa Yanga SC walifikiria kumsajili mshambuliaji huyo mrefu mkali wa mabao, anayechezea El Merreikh ya Sudan.
  Na baada ya Maximo kurejea Dar es Salaam juzi, naye amewaambia viongozi wa Yanga SC, anamtaka Traore, ili akate mchezaji mmoja wa kigeni kati ya viungo Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima, wote kutoka Rwanda au mshambuliaji Mganda Hamisi Kiiza. VIDEO; Traore akiichezea Mali dhidi ya China mechi ya kirafiki ya kimataifa ipo chini kabisa
  Mwenye kisu kikali atakula nyama; Mohamed Traore anagombewa na Yanga SC na Azam FC

  Maana yake Wabrazil, viungo Andrey Coutinho na Emerson Roque wako salama. Emerson ametua juzi kufanya majaribio, achukue nafasi ya Genilson Santos ‘Jaja’, aliyejitoa baada ya miezi tatu ya kusajiliwa kwa matatizo ya kifamilia.
  BIN ZUBEIRY inafahamu Maximo atakuwa na kikao na uongozi wa Yanga SC kujadili masuala mbalimbali ya maandalizi ya timu, ikiwemo usajili.
  Lakini wakati Maximo na viongozi wa Yanga SC wote wamevutiwa na Traore, tayari mchezaji huyo yuko katika mazungumzo na uongozi wa Azam FC, ambayo imeelezwa yanaendelea vizuri.
  Azam FC wana matumaini makubwa ya kumpata mchezaji huyo, ambaye kwa sasa analipwa dola za Kimarekani 180,000 (Sh. Milioni 300) kwa mwaka mbali na mshahara wa dola 10,000 (Sh. Milioni 17,000) kwa mwezi El Merreikh.
  Lakini habari zaidi zinasema, Traore aliyechoshwa na maisha ya Sudan, yuko tayari kwenda kucheza sehemu nyingine kwa fedha chini ya hizo anazolipwa Merreikh kwa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TRAORE ANASA RADA ZA YANGA SC, MAXIMO AWAAMBIA VIONGOZI; “NILETEENI KIFAA HICHO HARAKA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top