• HABARI MPYA

  Friday, November 28, 2014

  MOSOTI AWAGEUKIA SIMBA; AJIUNGA NA TUSKER FC

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  ALIYEKUWA beki wa Simba SC ya Tanzania, Donald Mosoti ametia mkataba wa miaka miwili na mabingwa mara kumi wa ligi kuu ya taifa la Kenya, Tusker FC.
  Kocha wa Tusker Francis Kimanzi aliliambia Bin Zubeiry kuwa amemsajili Mosoti kwa uzoefu wake na sasa anasubiri tu msimu ujao ufike aiwajibikie timu hiyo.
  “Tushamalizana na yeye kuhusiana na maswala ya mkataba. Tumeelewana na sasa kinachobakia ni mambo machache tu ili aruhusiwe kucheza msimu ujao”, alisema kocha wa zamani wa timu ya taifa la Kenya, Harambee Stars.
  Donald Mosoti (kulia) amesaini Mkataba na Tusker FC nchini Kenya

  Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu, Mosoti alithibitisha uhamisho huo huku akisisitiza kuwa ingekuwa vigumu kwake kurejea hivi karibuni Simba baada ya kutemwa mwishoni mwa mwezi wa nane pasi na kumfahamisha kwa wakati.
  Mlinzi huyo wa zamani wa Nairobi City Stars na Gor Mahia za Kenya alijiunga na Wekundu wa Msimbazi Desemba 2013 kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Amekuwa akifanya mazoezi na wanavileo hao wa Tusker.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOSOTI AWAGEUKIA SIMBA; AJIUNGA NA TUSKER FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top