• HABARI MPYA

  Friday, November 28, 2014

  PIGO ARSENAL, WILSHERE NJE MIEZI MINNE BAADA YA 'KUPIGWA KISU' JANA

  KLABU ya Arsenal inakabiliwa na baa la majeruhi, baada ya Jack Wilshere naye kutakiwa kuwa nje kwa miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu jana.
  Na kocha Arsene Wenger atalazimika kuingia sokoni Januari kununua wachezaji ili kupoza maumivu ya tatizo la majeruhi kikosini mwake. 
  Wilshere amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto baada ya kipigo cha Manchester United cha mabao 2-1 Uwanja wa Emirates Jumamosi iliyopita. Na Nahodha, Mikel Arteta pia anaweza asicheze tena mwaka huu baada ya kuumia Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund.
  Wilshere posted a picture of his ankle in a cast after the operation and insisted he will return soon
  Wilshere ameposti picha hii baada ya kufanyiwa upasuaji

  Kuuminia kwa Wilshere kunamfanya kocha Arsene Wenger awakose viungo wote watatu tegemeo, Aaron Ramsey, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky.
  Baada ya upasuaji huo, Wilshere akaposti picha Instagram akiwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba zoezi limekwenda vizuri.
  "Kifundo cha mwishowe kilihitaji upasuaji," ameandika. "Zoezi limekwenda vizuri na asante kwa mkuu James Calder (mpasuaji)!
  Wilshere was clearly in pain after the tackle and it is unlikely that he will be back for Arsenal before March
  Wilshere akiugulia maumivu baada ya kuumia na anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kabla ya Machi, mwakani
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO ARSENAL, WILSHERE NJE MIEZI MINNE BAADA YA 'KUPIGWA KISU' JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top