• HABARI MPYA

    Sunday, November 30, 2014

    MAN CITY PUNGUFU YAIFUMUA 3-0 SOUTHAMPTON

    LICHA ya kucheza pungufu baada ya Eliaquim Mangala kutolewa kwa kadi nyekundu, Manchester City imepata ushindi mnono ugenini wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa St Mary's, Yaya Toure aliifungia bao la kanza City dakika ya 51, kabla ya Mangala kutolewa kwa kadi ya pili ya njano dakika ya 74.
    Pamoja na kubaki wachache, mabingwa hao watetezi walifanikiwa kuongeza mabao kupitia kwa Frank Lampard aliyetokea benchi dakika ya 80 na Gael Clichy dakika ya 88.
    Beki Vincent Kompany alitolewa nje dakika za mwishoni baada ya kuumia, lakini City haikubadili mchezaji kwa kuwa ilikwishamaliza nafasi baada ya James Milner, Lampard na Martin Demichelis wote kutokea benchi kuchukua nafasi za Stevan Jovetic, Samir Nasri na Jesus Navas.  
    City's Eliaquim Mangala received a second booking for bringing down Shane Long just outside the penalty area
    Mchezaji wa City, Eliaquim Mangala akimchezea rafu Shane Long wa Southampton nje ya eneo la penalti iliyomponza kuonyeshwa kadi ya pili ya njano
    Toure skips past the challenge of Southampton midfielder Victor Wanyama in the first half at St Mary's
    Yaya Toure akimtoka kiungo wa Southampton, Victor Wanyama Uwanja wa St Mary's

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2854890/Southampton-0-3-Manchester-City-Yaya-Toure-Frank-Lampard-Gael-Clichy-earn-three-points.html#ixzz3KZDBBg44 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY PUNGUFU YAIFUMUA 3-0 SOUTHAMPTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top