• HABARI MPYA

  Friday, November 28, 2014

  DIAMOND NA YEMI ALADE WALIVYOMPA RAHA MAYWEATHER

  BONDIA Floyd Mayweather Jnr ameposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji, huku anasikiliza wimbo wa wasanii wa Afrika, Mtanzania Diamond Platnumz na Mnigeria Yemi Alade.
  Bingwa huyo wa dunia wa maraja matano tofauti ya uzito, ameposti video hiyo akifanyiwa masaji na mrembo huku muziki wa Diamond na Yemi Alade uitwao Johnny ukiwaliwaza. Mwanamichezo huyo tajiri zaidi duniani, ameposti video hiyo ikiwa imeambatana na ujumbe usemao: '#HAPPYTHANKSGIVING'.

  Wakati huo huo, Manny Pacquiao kwa mara nyingine amekumbushia pambano na mpinzani wake huyo ambaye hajawahi kupoteza pambano.
  Mayweather alimkebehi Mfilipino huyo baada ya ushindi wake wa pointi dhidi ya Chris Algieri kwa kuweka video kwenye Instagram ikimuonyesha Pacquiao akikalishwa chini kwa konde la Juan Manuel Marquez katika pambano la mwaka 2012.
  Bingwa huyo wa WBO uzito wa Welter alijibu kwa kusema: "Anatakiwa kuja kupambana na mimi tangu nidondoshwe kwa urahisi. Mashabiki wanastahili pambano hilo. Nafikiri ni wakati kujitokeza na kusema ndiyo,".
  Mayweather Jnr has been called out again by WBO Welterweight champion Manny Pacquiao
  Mayweather Jnr ametakiwa tena ulingoni na bingwa wa WBO uzito wa Welter, Manny Pacquiao
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIAMOND NA YEMI ALADE WALIVYOMPA RAHA MAYWEATHER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top