• HABARI MPYA

  Sunday, November 23, 2014

  LEWIS MPYA ASHINDA KO YA 10 MFULULIZO AKIMMALIZA MPINDANI RAUNDI YA TATU TU

  BONDIA Anthony Joshua anayetarajiwa kuwa Lennox Lewis mpya, amempiga mpinzani wake mkongwe Michael Sprott na kuweka rekodi ya kushinda mapambano 10 mfululizo kwa Knockout (KO) tangu aanze ngumi za kulipwa.
  Bingwa huyo wa Olimpiki alianza vizuri pambano hilo mjini Liverpool akitamba kuanzia dakika ya kwanza, akimshambulia mfululizo mpinzani wake kiasi cha kumlazimisha refa kuingilia kati kuwaachanisha.
  Akiwa na umri wa miaka 39, Sprott alionyesha hizi si zama zake tena za kufurukuta kwenye ndondi za uzito wa juu, akifanya vibaya katika pambano la sita baada ya kupigwa kwa KO Ranudi ya tatu usiku wa jana.
  Joshua made it 10 wins in as many fights with another impressive display on Saturday night
  Joshua amefikisha mapambano 10 mfululizo ya kushinda kwa KO
  Joshua celebrates as Sprott (right) sinks in his chair after another impressive night for the the former Olympic champion
  Joshua akishangilia baada ya kummaliza Sprott 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2845755/Anthony-Joshua-dispatches-Michael-Sprott-90-seconds-make-10-KOs-10-fights.html#ixzz3JrkTtq2i 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LEWIS MPYA ASHINDA KO YA 10 MFULULIZO AKIMMALIZA MPINDANI RAUNDI YA TATU TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top