• HABARI MPYA

  Wednesday, November 26, 2014

  MESSI AFIKISHA MABAO 74 LIGI YA MABINGWA BAADA YA HAT TRICK JANA

  MSHAMBULIAJI Lionel Messi amevunja rekodi ya mabao Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga hat-trick jana katika ushindi wa 4-0 dhidi ya APOEL mjini Nicosia na kufikisha jumla ya mabao 74 kwenye michuano hiyo.
  Nyota huyo wa Barcelona alimfikia mchezaji aliyekuwa anaongoza, Raul baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Ajax mapema Novemba, lakini mabao yake matatu ya jana yanamfanya awapiku wote.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi Messi amesema: "Nina furaha sana kuvunja rekodi hususan katika mashindano muhimu kama haya, lakini huu ulikuwa mchezo mkubwa kwetu mbali na rekodi zote,"amesema. 
  Lionel Messi celebrates after scoring his 73rd Champions League goal - and he went on to get another
  Lionel Messi akishangilia baada ya kutimiza mabao 73 kwenye Ligi ya Mabingwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AFIKISHA MABAO 74 LIGI YA MABINGWA BAADA YA HAT TRICK JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top