• HABARI MPYA

  Monday, November 24, 2014

  AZAM TV YAZINDUA MTONYO CHAP CHAP, NI MWEZI MZIMA WA WATU KUVUNA MAHELA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Azam Media Limited leo imezindua promosheni ya kila mwaka iitwayo Mtonyo Chap Chap, ambayo itafikia tamati Desemba 24, mwaka huu. 
  Mtonyo Chap Chap inawapa fursa wateja wa Azam TV kurejeshewa thamani ya matumizi yao ya ving’amuzi vya kampuni hiyo.
  Ili kuingia katika droo hiyo, watu wanatakiwa kununua ving’amuzi kipya vya Azam TV na kukiwekea malipo ya mwezi.
  Kutakuwa na jumla ya washindi 100 watakaopatikana katika kipindi chote cha kampeni hiyo ambao watakuwa wakitangazwa kila wiki kupitia kwenye vyombo habari, mbalimbali kama vituo vya Radio, Televisheni, Magazeti na blogs. Wiki ya kwanza, watangazwa washindi 15, kama ambavyo itakuwa katika wiki ya pili, wakati ya tatu watatangazwa washindi  20 kabla ya wiki ya mwisho kutangazwa washindi 50.
  Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torringotn kulia akizungumza na waandishi wa Habari leo, makao makuu ya kampuni hiyo, TAZARA, barabara la Nyerere na Mandela, Dar es Salaam leo kuhusu promosheni ya Mtonyo Chap Chap ya Azam TV, ambayo imeanza leo na itaendelea hadi Desemba 24, mwaka huu. Wengine kulia, Ofisa Masoko na mauzo, Shah Mrisho na Meneja Masoko na Mauzo, Mgope Kiwanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM TV YAZINDUA MTONYO CHAP CHAP, NI MWEZI MZIMA WA WATU KUVUNA MAHELA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top