• HABARI MPYA

  Saturday, November 22, 2014

  WENGER AMPELEKA PEMBENI WELBECK KUMPSHA GIROUD KATIKATI

  KOCHA Arsene Wenger amedokeza kwamba mshambuliaji Danny Welbeck atahamishiwa wingi ya kushoto katika mechi dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester United jioni ya leo ili kumpisha Olivier Giroud aliyererejea baada ya kuwa fiti.
  Arsenal inamkaribisha tena Giroud baada ya miezi mitatu ya kuwa nje ya Uwanja akiguza kifundo chake cha mguu, lakini kurejea kwake kunampasua kichwa kocha Wenger juu ya upangaji wa timu.
  Welbeck hakufanya siri hata kidogo juu ya nia yake ya kutumiwa kama mshambuliaji wa kati tangu amewasili kutoka Old Trafford katika usajili wa siku ya mwisho ya kufungwa pazia na ameweza kuifungia mabao matano Arsenal akicheza badala ya Giroud.France international Giroud trains at London Colney ahead of United's visit to the Emirates
  Mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa, Giroud akiwa mazoezini viwanja vya Colney, London kujiandaa na mcchi dhidi ya United Uwanja wa Emirates
  Wenger says that Welbeck was never given any guarantees that he would play centrally
  Wenger amesema kwamba Welbeck hakuwahi kupewa uhakika wa kucheza kama mshambuliaji wa kati

  Pamoja na hayo, Wenger amesema kwamba Welbeck hakuwahi kupewa uhakika wa kucheza kama mshambuliaji wa kati baada ya kusajiliwa Arsenal. "Welbeck anaweza kucheza katika nafasi tofauti pale mbele, sifikirii hiyo itamzuia kuendelea kufunga,"amesema Wenger.
  Kocha wa United, Louis van Gaal aliweka wazi kwamba alimuacha Welbeck aondoke kwa sababu hakuwa nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER AMPELEKA PEMBENI WELBECK KUMPSHA GIROUD KATIKATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top