• HABARI MPYA

  Monday, November 24, 2014

  MSIBA CHELSEA, KOCHA WA ZAMANI AFARIKI DUNIA

  Pumzika kwa amani John Neal
  KOCHA wa zamani wa Chelsea, John Neal amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, vinara hao wa Ligi Kuu England wametangaza leo.
  Neal, alimrithi shujaa wa hat trick katika Kombe la Dunia mwaka 1966, Geoff Hurst Uwanja wa Stamford Bridge mwaka 1981, aliiongoza klabu hiyo kutwaa taji la pili mwaka 1984 kabla ya kustaafu kwa sababu ya maradhi mwaka mmoja baadaye.
  "Klabu ya soka ya Chelsea ina huzuni mno na kifo cha John Neal, mmoja kati ya makocha kipenzi na alma katika historia yetu. Klabu inatuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya John na marafiki," imesema taarifa ya klabu.
  "John atakumbukwa daima Chelsea kwa kuiongoza timu wakati tupo ngazi za chini,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSIBA CHELSEA, KOCHA WA ZAMANI AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top