• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  BULGARIA YAMTUPIA VIRAGO LUBOSLAV PENEV BAADA YA MATOKEO MABAYA KUFUZU EURO 2016

  Luboslav Penev amefukuzwa kazi Bulgaria
  BULGARIA imemfukuza kocha Luboslav Penev baada ya mwanzo mbaya kwenye kampeni za kufuzu Euro 2016, Umoja wa Soka wa nchi hiyo umetangaza leo.
  "Tumevunja Mkataba na Penev," amesema Rais wa BFU, Borislav Mihaylov katika Mkutano na Waandishi wa Habari. "Timu haijafanya vizuri na tunakaribia kupoteza nafasi ya kufuzu kwenye Fainali za Euro 2016, pamoja na kwamba timu mbili za juu zinafuzu moja kwa moja.
  "Natumai tutakuwa na kocha mpya wakati wa mwaka mpya. Naweza kukuambia kocha mpya hatakuwa mgeni,"amesema.
  Penev, mwenye umri wa miaka 48, aliongeza Mkataba wa miaka miwili Novemba mwaka jana, lakini matokeo mabaya kwenye mechi za kufuzu Euro 2016 yanamuondoa kazini baada ya miaka mitatu.
  Bulgaria, ambayo imeshindwa kufuzu kwenye mashindano yoyote makubwa tangu mwaka 2004, inashika nafasi ya nne katika Kundi H ikiwa na pointi nne baada ya mechi kibao, ikizidiwa pointi sita na vinara Croatia na tano na Italia na Norway.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BULGARIA YAMTUPIA VIRAGO LUBOSLAV PENEV BAADA YA MATOKEO MABAYA KUFUZU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top