• HABARI MPYA

  Thursday, November 20, 2014

  MBEYA CITY WAMIPIGIA MAGOTI KOCHA MWAMBUSI, AWAPA MASHARTI WAKIYAKUBALI ATAREJEA KAZINI

  Na Emanuel Madafa, MBEYA
  SIKU chache baada ya kocha, Juma Mwambusi kutangaza kujiuzulu, kumeibuka tetesi kwamba huenda kocha huyo akarejea kukinoa kikosi hicho endapo uongozi utaridhia baadhi ya masharti aliyoyapendekeza kocha huyo.
  Habari za ndani zilizotufikia zinasema kwamba uongozi wa klabu hiyo, umeonyesha imani kubwa na kocha Mwambusi hivyo kumtaka kurejea tena kikosini.
  Moja ya masharti ambayo yamewekwa bayana na kocha huyo kwamba ni lazima uongozi kuyatekeleza  ni kwamba  endapo atarejea kikosini asingependa uongozi kumuingilia kwenye majukumu yake ya kiutendaji.
  Pia uongozi, huo umetakiwa kuweka mipaka kwa mashabiki ambao kwa sasa wameonekana kuitawala klabu hiyo hadi kufikia hatua ya kuingilia utendaji wa mwalimu kwa  kumtaka kupanga wachezaji wanaowataka wao.
  Akizungumzia hilo, Meya wa  Jiji la Mbeya, Athanas  Kapunga ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya timu hiyo, amesema  suala la kocha kujiuzulu bado linafanyiwa kazi na uongozi na kwamba vikao vya kulijadili bado  vinaendelea kufanyika.
  Mwambusi anaweza kurejea Mbeya City
  Amesema bado  wanaendelea na vikao  vya ndani hivyo suala la kocha Mwambusi liko mezani nakwamba  hivi sasa ndio wanaelekea  kulijadili na kulitolea tamko kesho Nov 21 katika mara baada ya kukamilika kwa baraza la Madiwani.
  Hata hivyo masharti ya kocha huyo yametajwa kuwa huenda yakawagharimu baadhi ya viongozi. Imehamishwa kutoka http://www.jamiimoja.blogspot.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY WAMIPIGIA MAGOTI KOCHA MWAMBUSI, AWAPA MASHARTI WAKIYAKUBALI ATAREJEA KAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top