• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    BEKI AZAM APATA AJALI, GARI LAKE LAGONGANA NA BODABODA KIJITONYAMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    Beki wa Azam, Erasto Nyoni
    BEKI wa Azam FC, Erato Edward Nyoni amepata ajali eneo la Kijitonyama, Dar es Salaam jioni ya leo, baada ya gari lake kugongana na pikipiki.
    Walioshuhudia tukio hilo, wanasema mwendesha pikipiki aliingia vibaya barabarani na kugongana na gari la beki huyo kimataifa wa Tanzania.
    Hata hivyo, baada ya tukio hilo, mwendesha bodaboda huyo aliwapigia simu wenzake na kumiminika kwa wingi eneo la tukio kwa ajili ya kumpiga mchezaji huyo.
    Bahati nzuri, Erasto naye aliwahi kuwataarifu viongozi wa klabu yake, ambao walichukua hatua ya kumfuata haraka eneo la tukio ili kumtoa salama.
    Hiyo inatokana na desturi moja mbaya ya waendesha bodaboda na bajaji Dar es Salaam kuchukua sheria mkononi baada ya ajali inayomuhusisha mwenzi wao, kumpiga kama mwizi aliyegongana naye, pasipo kujali nani alikuwa ana makosa.   
    Taarifa zaidi za tukio hilo zinatarajiwa kutolewa na jeshi la Polisi Kinondoni, Dar es Salaam kesho.

    Gari la Erasto Nyoni baada ya kugongana na bodaboda
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI AZAM APATA AJALI, GARI LAKE LAGONGANA NA BODABODA KIJITONYAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top