• HABARI MPYA

    Wednesday, January 09, 2019

    SALAH MWANASOKA BORA AFRIKA, ONYANGO AWA KIPA BORA

    MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2018 kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya miezi 12 mizuri.
    Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwasaidia Wekundu hao kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei mwaka jana na amekuwa chachu ya mafanikio ya Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England hadi sasa ikiwa inaongoza. 
    Katika sherehe zilizofanyika mjini Dakar, Senegal, usiku wa jana, Salah ametetea tuzo aliyoitwaa miezi 12 iliyopita.
    Salah aliweka rekodi ya mabao msimu wa 2017/18 kwa kufunga mabao 32 kwenye Ligi Kuu nya England na 44 jumla katika mashindano yote.


    Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, George Weah akimkabidhi Mohamed Salah tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika jana mjini Dakar, Senegal PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    Pia alifunga mabao mawili katika fainali za Kombe la Dunia mwaka jana ambazo zilikuwa za kwanza kwa Misri baada ya miaka 28.
    Salah amemshinda mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na nyota wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang. 
    Salah alikabidhiwa tuzo huyo na gwiji wa soka Afrka na Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, George Weah ambaye pia ni Rais wa Liberia.
    Na akateuliwa kwenye kikosi bora cha Afrika 'Africa Best XI 2018' sambamba na  Mane, Naby Keita, Aubameyang, Riyad Mahrez wa Manchester City, Eric Bailly wa Manchester United, Serge Aurier wa Tottenham, Medhi Benatia wa Juventus, Kalidou Koulibaly wa Napoli, Thomas Partey wa Atletico Madrid na kipa Mganda, Denis Onyango wa Mamelodi Sundowns. 

    WASHINDI WOTE WA TUZO ZA AFRIKA
    Mwanasoka Bora Kiume
    Mohamed Salah (Egypt & Liverpool)
    Mwanasoka Bora wa Kike
    Chrestinah Thembi Kgatlana (Afrika Kusini & Houston Dash)
    Mwanasoka Bora Chipukizi
    Achraf Hakimi (Morocco & Borussia Dortmunmd)
    Kocha Bora wa Kiume
    Herve Renard (Morocco)
    Kocha Bora wa Kike
    Desiree Ellis (Afrika Kusini)
    Timu Bora ya Taifa ya Wanaume
    Mauritania 
    Timu Bora ya taifa ya wanawake
    Nigeria
    Tuzo ya Platinum
    Mheshimiwa Macky Sall (Rais wa Senegal)
    Rais Bora wa Shirikisho
    Fouzi Lekjaa
    Bao Bora la Mwaka

    Chrestinah Thembi Kgatlana (Afrika Kusini & Houston Dash)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH MWANASOKA BORA AFRIKA, ONYANGO AWA KIPA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top