• HABARI MPYA

  Sunday, July 08, 2018

  SIMBA SC YAIPIGA AS PORTS 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la mshambuliaji mpya, Mohammed Rashid limeipeleka Simba SC fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya AS Ports ya Djibouti Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Rashid aliyesajiliwa kutoka Tanzania Prisons mwezi uliopita alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti ka kiutaalamu akimchambua kipa hodari wa Ports, Lumiya Sulait baada ya pasi ya beki Mghana, Nicholas Gyan aliyepanda kusaidia mashambulizi.
  Na Rashid alifunga bao hilo dakika sita tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake mpya Simba SC, Adam Salamba aliyesajiliwa mwezi uliopita pia kutoka Lipuli FC ya Iringa.
  Mohammed Rashid (kulia) akikimbia kushangilia na Meddie Kagere baada ya kufunga bao pekee leo

  Meddie Kagere (kulia) akiwatoka wachezaji wa AS Ports leo Uwanja wa Taifa

  Ports watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nzuri za kufunga kipindi cha kwanza, ikiwemo ile ya dakika ya 44 ambayo mshambuliaji Doualeh Mohamoud Elabeh alipiga nje akiwa amebaki yeye na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.
  Kwa matokeo hayo sasa, Simba itakut ana na mshindi kati ya Singida United na JKU zitakazomenyana kesho katika Nusu Fainali Jumatano Uwanja wa Taifa tena. Gor Mahia ya Kenya baada ya kuitoa Vipers ya Uganda kwa kuichapa mabao 2-1 katika mchezo uliotangulia jioni ya leo itasubiri mshindi kati ya Azam FC na Rayon Sport kukutana naye Nusu Fainali.
  Na baada ya mashindano hayo, Simba SC ikamchukua mshambuliaji Meddie Kagere ambaye Jumatano atacheza dhidi ya timu yake ya zamani.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Deogratius Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, Pascal Wawa, James Kotei, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk43, Mwinyi Kazimoto, Meddie Kagere, Adam Salamba/Mohammed Rashid dk59 na Mercel Kaheza/Rashid Juma dk68. 
  AS Ports: Lumiya Sulait, Mohammed Bourhan, Franck Ndayisenga, Ibrahim Aden Warsama, Mohammed Abdourahman/Mohamed Salem dk80, Wais Daoud Wais, Hamza Abdi Idleh, Moussa Helem Mohamed, Bangnie Guessebo Junior/Abdoulrazak Mahamoud dk78, Doualeh Mohamoud Elabeh na Mahdi Houssein Mahabeth.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIPIGA AS PORTS 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top