• HABARI MPYA

  Monday, July 09, 2018

  MTIBWA SUGAR WAPEWA VIWANJA KWA KUTWAA ASFC, DILUNGA ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  MKUU wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe amewapa wachezaji wa Mtibwa Sugar zawadi ya viwanja vilivyopo mkoani humo ikiwa ni zawadi baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwaka huu.
  Kebwe ametoa zawadi hiyo jana kwenye Hafla ya utoaji wa Tuzo za Klabu ya Mtibwa Sugar iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya New Afrika iliyopo Posta Mjini Dar es Salaam.
  Katika Tuzo hizo zilizokuwa na vipengele mbalimbali, Hassan Dilunga alishinda Tuzo ya mchezaji bora wa msimu ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar ambapo katika  kipengele hicho  Dilunga alikuwa anawania na  Salum Kihimbwa, Cassian Ponela, Shaaban Nditi na Dickson Daud.

  Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe (kushoto) akimkabidhi Hassan Dilunga tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu Mtibwa Sugar

  Dilunga pia amechukua tuzo ya mfungaji bora kwa mabao yake tisa aliyofunga msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na manne kwenye ASFC.
  Tuzo ya Goli Bora la msimu ilienda kwa Salum Kihibwa goli alilowafunga Singida United kwenye mechi ya fainali za Kombe la Azam Sports Federation Cup, Kihimbwa amewashinda Ally Makalani, Ismail Muhesa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.
  Benedict Tinocco amechukua Tuzo ya kipa bora wa msimu ndani ya kikosi hicho, akiwashinda Shaaban Kado na Abdallah Makangana.
  Tuzo ya mchezaji bora anayechipukia imeenda kwa Salum Kihibwa, Tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu bora imeenda kwa Hassan Suleyman {IS-Haka}.
  Tuzo ya mchezaji mwandamizi alichukua Shabani Mussa Nditi pamoja ma Tuzo ya mchezaji aliyecheza dakika nyini alichukua Dickson Daud,Tuzo kwa Benchi la ufundi ilienda kwa Kocha Zuber Katwila na Patrick Mwangata
  Kwa upande wa Tuzo za U-20; Tuzo ya mchezaji bora alichukua Onesmo Justin Mayaya,Aboutwalib Mshery alichukua Tuzo ya Golikipa bora,Tuzo ya Goli bora ilienda kwa Richard William,mchezaji aliyecheza dakika nyingi alichukua Kibwana Ally Shomary.
  Tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu ilienda kwa Dickson Job pamoja na Tuzo kwa Benchi la ufundi ilienda kwa Kocha Vincent Barnabas Salamba
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAPEWA VIWANJA KWA KUTWAA ASFC, DILUNGA ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top