• HABARI MPYA

    Sunday, July 08, 2018

    LIPULI YASAJILI WANNE KWA MPIGO WAKIWEMO GALLAS, MIRAJ SHEVCHENKO NA NONGA



    Na Mwandishi Wetu, IRINGA
    TIMU ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa leo imekamilisha usajili wa wachezaji wapya wanne kutoka timu tofauti, wakiwemo nyota wawili wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam.
    Wachezaji hao ni pamoja na washambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Paul John Nonga kutoka Mwadui FC ya Shinyanga aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja na Issa Ally Rashid, mchezaji huru ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.  
    Wengine ni beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, William Lucian ‘Gallas’ kutoka Ndanda FC ya Mtwara na mshambuliaji Miraj Madenge ‘Shevchenko’ kutoka Mwadui FC ambao wote kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

    Paul Nonga amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Lipuli FC ya Iringa kutoka Mwadui FC ya Shinyanga  
    William Lucian ‘Gallas’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Lipuli FC ya Iringa kutoka Ndanda FC ya Mtwara 
    Miraj Madenge ‘Shevchenko’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Lipuli FC ya Iringa Mwadui FC ya Shinyanga

    Gallas na Shevcheko wanakwenda kuungana tena na Suleiman Matola, aliyekuwa kocha wao kuanzia timu ya vijana ya Simba SC chini ya umri wa miaka 20, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na baadaye kuchwa mwaka 2014.
    Na Nonga anakwenda kukutana tena na mshambuliaji Malimi Busungu, ambaye walicheza naye Yanga SC miaka mitatu iliyopita chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kabla ya wote kuondoka kutokana na kutopata nafasi kikosi cha kwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIPULI YASAJILI WANNE KWA MPIGO WAKIWEMO GALLAS, MIRAJ SHEVCHENKO NA NONGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top