• HABARI MPYA

  Sunday, July 08, 2018

  GOR MAHIA YATANGULIA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUIPIGA VIPERS 2-1

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Gor Mahia ya Kenya imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Vipers ya Uganda leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Sasa Gor Mahia ya kocha Muingereza, Dylan Kerr itasubiri mshindi kati ya Azam FC na Rayon Sport ya Rwanda zitakazomenyana kesho ikutane naye katika mechi ya Nusu Fainali.  
  Haukuwa ushindi mwepesi kwa Gor Mahia, kwani ilibidi watoke nyuma baada ya Vipers kutangulia kwa bao la Thadeo Lwanga dakika ya 17 kwa shuti la mbali na kumtungua kipa.
  Kiungo wa Gor Mahia, George Odhiambo 'Blackberry' (kulia) akiondoka na mpira dhidi ya mchezaji wa Vipers, Ibrahim Kiyemba 

  Gor Mahia wakazinduka na kusawazisha kwa bao la Francis Mustafa dakika ya 48 aliyeunganisha krosi ya Innocent Wafula, kabla ya kufunga na la pili dakika ya 75 hivyo kuifungisha virago timu ya Uganda.
  Kikosi cha Gor Mahia kilikuwa: Boniface Oluoch, Innocent Wafula, Godfrey Walusimbi, Haron Shakava, Ernest Wendo/Francis Kahata dk44, Charles Momanyi, Humphrey Mieno, Jacques Tuyisenge, George Odhiambo ‘Blackberry’ na Francis Mustafa/Eiphraim Guikana dk86. 
  Vipers: Bashir Sekagya, Dan Sserunkuma, Bashir Asiku, Geoffrey Wasswa, Steven Mukwala/Brian Nkuubi dk46, Milton Karisa, Ibrahim Kiyemba, Tadeo Lwanga, Yayo Lutimba Kato/Pius Wanji dk81, Rahmat Ssenfuka na Duncan Sseninde.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOR MAHIA YATANGULIA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUIPIGA VIPERS 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top