• HABARI MPYA

    Tuesday, July 07, 2015

    BARCELONA YAZIPIGA BAO CHELSEA NA MAN UNITED, ARDA TURAN ATUA CAMP NOU

    KLABU ya Barcelona imefikia maubaliano na Atletico Madrid juu ya kumsajili kiungo Arda Turan kwa Pauni Milioni 29. 
    Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 alizivutia pia Chelsea na Manchester United, lakini Barcelona imeshinda mbio za kuwania saini yake. 
    Barcelona italipa Pauni Milioni 24 mbele na nyingine Pauni Milioni 5 zitalipwa baadaye kufuatia mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uturuki kusaini Mkataba wa miaka mitano.

      

    Barcelona imeposti picha hii ya 'kubumba' ya Arda Turan akiwa na jezi ya klabu hiyo baada ya kutangaza kumsajili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA YAZIPIGA BAO CHELSEA NA MAN UNITED, ARDA TURAN ATUA CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top