• HABARI MPYA

  Sunday, February 25, 2024

  TABORA UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 NA FOUNTAIN GATE


  WENYEJI, Tabora United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Tabora United walitangulia na bao la Yahya Mbegu dakika ya 53, kabla ya John Nakibinge kuisawazishia Singida Fountain Gate dakika ya 83.
  Kwa matokeo hayo, Singida Fountain Gate wanafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya sita, wakati Tabora United wamefiisha pointi 18 na kusogea nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 NA FOUNTAIN GATE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top