• HABARI MPYA

  Saturday, February 24, 2024

  WANIGERIA WAIKANDA MAN UNITED FULHAM YASHINDA 2-1


  WENYEJI, Manchester United wamechapwa mabao 2-1 na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Fulham yamefungwa na Wanigeria yote, beki Calvin Chinedu Bassey mzaliwa wa Italia dakika ya 65 na mshambuliaji Alexander Chuka Iwobi dakika ya 90 na ushei, huku bao pekee la Manchester United likifungwa na beki Muingereza, Jacob Harry Maguire dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Fulham inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya 12, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 44 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WANIGERIA WAIKANDA MAN UNITED FULHAM YASHINDA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top