• HABARI MPYA

  Sunday, February 04, 2024

  CUNHA APIGA HAT-TRICK WOLVES YAICHAPA CHELSEA 4-2 STAMFORD BRIDGE


  MSHAMBULIAJI Mbrazil, Matheus Cunha amefunga mabao matatu kuiwezesha Wolverhampton Wanderers kuichapa Chelsea 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Cunha amefunga mabao hayo dakika za 22, 63 na 82, wakati bao lingine la Wolves limefungwa na beki Mfaransa, Axel Disasi aliyejifunga dakika ya 43, wakati mabao ya Chelsea yamefungwa na Cole Palmer dakika ya 19 na Thiago Silva dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Wolves inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya 10, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 31 na inashukia nafasi ya 11, baada ya wote kucheza mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CUNHA APIGA HAT-TRICK WOLVES YAICHAPA CHELSEA 4-2 STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top