• HABARI MPYA

  Saturday, February 17, 2024

  MUDATHIR APIGA MBILI YANGA YAICHAPA KMC 3-0 MORO


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Nyota ilikuwa ya kiungo Mudathir Yahya Abbas ‘Zanzibar Greatest’ aliyefunga mabao mawili dakika ya kwanza na ha 54, huku bao la tatu likiwekwa nyavuni na kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacôme Zouzoua dakika ya 59.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu mbele ya watani, Simba SC wenye pointi 36 na Azam FC pointi 35 baada ya wote kucheza mechi 15.
  Kwa upande wao KMC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 22 za mechi 16 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUDATHIR APIGA MBILI YANGA YAICHAPA KMC 3-0 MORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top