TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imetupwa nje ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia licha ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zambia katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Serengeti Girls leo limefungwa na Melkia William na kwa matokeo hayo Tanzania inatolewa kwa jumla ya mabao 5-1 kufuatia kuchapwa 5-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi ya wiki iliyopita Uwanja wa Nkoloma Jijini Lusaka.
Sasa Zambia itakutana na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Cameroon katika Raund ya Tatu.
Kutakuwa na Raundi ya Nne na ya mwisho na washindi watatu ndiyo wataiwakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitafanyika Jamhuri ya Dominican.
0 comments:
Post a Comment