• HABARI MPYA

  Friday, February 16, 2024

  KAGERA SUGAR YABANWA, SARE 1-1 NA MASHUJAA KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa alianza kuifungia Kagera Sugar dakika ya 62, kabla ya mshambuliaji mzawa, Relliant Lusajo kuisawazishia Mashujaa FC dakika ya 79.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 10, wakati Mashujaa imetimiza pointi 11 na yenyewe inabaki nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YABANWA, SARE 1-1 NA MASHUJAA KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top