• HABARI MPYA

  Friday, February 02, 2024

  MAN UNITED YASHINDA 4-3 DHIDI YA WOLVERHAMPTON MOLINEUX


  TIMU ya Manchester United imepata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Molineux, Wolverhampton, West Midlands.
  Mabao ya Manchester United yalifungwa na Marcus Rashford dakika ya tano, Rasmus Hojlund dakika ya 22, Scott McTominay dakika ya 75 na Kobbie Mainoo dakika ya 90+7, wakati ya Wolves yalifungwa na Pablo Sarabia kwa penalti dakika ya 71, Max Kilman dakika ya 85 na Pedro Neto dakika ya 90+5.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 35 na kusogea nafasi ya saba, wakati Wolverhampton Wanderers inabaki na pointi zake 29 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YASHINDA 4-3 DHIDI YA WOLVERHAMPTON MOLINEUX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top