• HABARI MPYA

  Thursday, February 22, 2024

  LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA LUTON 4-1 ANFIELD


  TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kushinda 4-1 dhidi ya Luton Town katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Chiedozie Ogbene alianza kuifungia Luton Town dakika ya 12, kabla ya Liverpool kuzinduka na mabao ya Virgil van Dijk dakika ya 56, Cody Gakpo dakika ya 58, Luis Diaz dakika ya 71 na  Harvey Elliott dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 60 katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 56 za mechi 25, wakati Luton Town inabaki na pointi zake 20 za mechi 25 nafasi y 18 kwenye Ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa a msimu tatu zitashuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA LUTON 4-1 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top