• HABARI MPYA

  Tuesday, February 06, 2024

  FODEN APIGA HAT-TRICK MAN CITY YAICHAPA BRENTFORD 3-1


  TIMU ya Manchester City jana imetoka nyuma na kuwachapa wenyeji , Brentford City mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex.
  Brentford walitangulia kwa bao la Neal Maupay dakika ya 21, kabla ya Phil Foden kufunga mfululizo dakika ya 45,53 na 70 hat trick ambayo imewarejesha nafasi ya pili mabingwa hao watetezi.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 49 katika mchezo wa 22 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili tu Liverpool ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Arsenal ni ya tatu ikiwa na pointi 49 pia za mechi 23.
  Kwa upande wao Brentford City baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 22 za mechi 22 nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FODEN APIGA HAT-TRICK MAN CITY YAICHAPA BRENTFORD 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top