• HABARI MPYA

  Sunday, February 11, 2024

  TABORA UNITED YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO 1-1 MWINYI


  WENYEJI, Tabora United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mshambuliaji hatari raia wa Ghana, Eric Okutu alianza kuifungia Tabora United dakika ya 11, kabla ya kiungo mzawa, Pius Buswita kuisawazishia Namungo FC dakika ya 37.
  Kwa matokeo hayo, Namungo FC wanafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya saba na Tabora United wanatimiza pointi 16, ingawa wanabaki nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO 1-1 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top