• HABARI MPYA

  Monday, February 05, 2024

  YANGA SC YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA DODOMA JIJI 1-0 CHAMAZI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mudathir Yahya Abbas ‘Zanzíbar Greatest’ dakika ya 85 akimalizia pasi nzuri ya beki wa kushoto, Nickson Kibabage baada ya wawili hao wote kutokea benchi kipindi cha pili.
  Yanga inafikisha pointi 34 na kurejea juu ya msimamo wa Ligi, ikiizidi pointi tatu Azam FC baada ya wote kucheza mechi 13, wakifuatiwa na Simba SC yenye pointi 26 za mechi 11 nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA DODOMA JIJI 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top