• HABARI MPYA

  Sunday, February 25, 2024

  AZAM FC YAAMBULIA SARE YA 1-1 KWA PRISONS MBEYA


  WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Tanzania Prisons walitangulia na bao la Samson Mbangula dakika ya tano, kabla ya kiungo Feisal Salum kuisawazishia Azam FC dakika ya 54 kwa penalti.
  Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya saba, wakati Azam FC inafikisha pointi 37 na inabaki nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAAMBULIA SARE YA 1-1 KWA PRISONS MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top