MCHEZO wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya Mtibwa Sugar na Simba SC uliopangwa kufanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Jumapili umeahirishwa.
Taarifa ya Bodi ya Ligi leo imesema kwamba mchezo huo umeahirishwa kwa sababu Simba SC wanatakiwa kusafiri kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, ASEC Mimosas Ijumaa Jijini Abidjan.
0 comments:
Post a Comment