• HABARI MPYA

    Sunday, February 04, 2024

    ARSENAL YAICHAPA LIVERPOOL 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA


    WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
    Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 14, Gabriel Martinelli dakika ya 67 na Leandro Trossard dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Liverpool alijifunga Gabriel Magalhães dakika ya 45 na ushei.
    Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 49 na kupanda nafasi ya pili, sasa ikizidiwa pointi mbili tu na Liverpool baada ya wote kucheza mechi 23 wakiwa mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 46 za mechi 21.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA LIVERPOOL 3-1 NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top