• HABARI MPYA

  Wednesday, February 14, 2024

  MANCHESTER CITY YAWAKANDA COPENHAGEN 3-1 PALE PALE DENMARK


  MABINGWA watetezi, Manchester City jana wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, huku FC Copenhagen katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Parken Jijni Copenhagen, Denmark.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Kevin De Bruyne dakika ya 10, ' Bernardo Silva dakika ya 45 na Phil Foden dakika ya 90 na ushei, wakati la Copenhagen limefungwa na Magnus Mattsson dakika ya 34.
  Timu hizo zitarudiana Machi 6 Uwanja wa Etihad Jijini Manchester na mshindi wa jumla atakwenda Robó Fainali.
  Mechi nyingine ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa jana, Real Madrid waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, RB Leipzig bao pekee la  Brahim Díaz dakika ya 48 Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig.
  Nao watarudiana Machi 6 Uwanja wa   Santiago Bernabéu Jijini Madrid na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAWAKANDA COPENHAGEN 3-1 PALE PALE DENMARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top