• HABARI MPYA

  Sunday, February 04, 2024

  IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI ZATINGA NUSU FAINALI AFCON


  WENYEJI, Ivory Coast wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mali katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 usiku wa jana Uwanja wa Bouaké mjini Bouaké.
  Kiungo wa Red Bull Salzburg ya Ausrtia, Nene Dorgeles alianza kuifungia Mali dakika ya 71, lakini mshambuliaji wa Brighton & Hove Albion ya England, Simon Adingra akaisawazishia Ivory Coast dakika ya 90.
  Baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, mchezo huo ukaenda kwenye dakika 30 nyongeza, ambako  mshambulaji wa Reims ya Ufaransa, Oumar Diakité aliwafungia wenyeji bao la ushindi dakika ya 120.


  Katika mchezo mwingine wa Nusu Fainali jana, Afrika Kusini iliitoa Cape Verde kwa penalti 2-1 kufuatia sare ya bila kufungaa ndani ya dakika 120, huku Ronwen Hayden Williams akiweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kuokoa penalti nne katika AFCON Kihistoria.
  Kipa huyo wa Mamelodi Sundwons, aliokoa penalti za Bebé, Willy Semedo, Laros Duarte, Patrick Andrade huku ya Bryan Teixeira pekee ndiyeo ilimpita na kutinga nyavuni.
  Waliofunga pennalti za Bafana Bafana ni Teboho Mokoena na Mothobi Mvala, huku Zakhele Lepasa na Aubrey Modiba wakikosa pia upande wa Afrika Kusini.
  Sasa Afrika Kusini itakutana na Nigeria, wakati Ivory Coast itacheza na DRC katika Nusu Fainali ambazo zitapigwa Jumatano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IVORY COAST NA AFRIKA KUSINI ZATINGA NUSU FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top