• HABARI MPYA

  Thursday, February 29, 2024

  NI LIVERPOOL NA MAN UNITED ROBO FAINALI FA ENGLAND


  VIGOGO, Chelsea, Manchester United, Manchester City na Liverpool wamefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali Kombe la FA England.
  Manchester City juzi waliwatandika wenyeji, Luton Town mabao 6-2 Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire, mshambuliaji Mnorway, Erling Braut Haaland akifunga mabao matano dakika ya tatu, 18, 40, 56 na 58.
  Bao lingine la Manchester City lilifungwa na kiungo Mcroatia, Mateo Kovačić, huku mabao yote ya Luton Town yakifungwa na kiungo Muingereza, Jordan Charles Clark dakika ya 45 na 52. 
  Jana Chelsea ikaichapa Leeds United 3-1 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya Chelsea yalifungwa na mshambuliaji Msenegal, Nicolas Jackson dakika ya 15, winga wa Ukraine, Mykhailo Mudryk dakika ya 37 na kiungo Muingereza, Conor John Gallagher, wakati ya Leeds United yalifungwa na mshambuliaji Mspaniola, Mateo Joseph dakika ya nane na 59.
  Nayo Manchester United ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest bao pekee la Casemiro dakika ya 89 Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.
  Liverpool ikakamilisha safari ya vigogo nane bora kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Southampton, mabao ya Lewis Koumas dakika ya 44, Jayden Danns dakika ya 73 na 88 Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mechi za Robo Fainali zitapigwa Jumamosi ya Machi 16 Wolverhampton Wanderers dhidi ya Coventry City, Manchester United na Liverpool, Chelsea na Leicester City na Manchester City dhidi ya Newcastle United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI LIVERPOOL NA MAN UNITED ROBO FAINALI FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top