• HABARI MPYA

  Sunday, February 25, 2024

  KAGERA SUGAR YAICHAPA IHEFU SC 2-1 KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 24 na beki wa kulia, mzawa Dickson Mhilu dakika ya 76, huku bao pekee la Ihefu SC limefungwa na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nane, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake 19 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA IHEFU SC 2-1 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top