• HABARI MPYA

  Sunday, February 11, 2024

  ARSENAL YAICHAPA WEST HAM UNITED 6-0 LONDON


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na William Saliba dakika ya 32, Bukayo Saka mawili dakika ya 41 kwa penalti na dakika ya 63, Gabriel Maghaelhas dakika ya 44, Leandro Trossard dakika ya 45 na Declan Rice dakika ya 65.
  Kwa ushindi Arsenal inafikisha pointi 52 katika mchezo wa 24, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa wastani wa mabao na Manchester City ambao pia wana mchezo mmoja mkononi.
  Kwa upande wao West Ham United baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 36 za mechi 24 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA WEST HAM UNITED 6-0 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top