• HABARI MPYA

  Saturday, February 17, 2024

  LIVERPOOL YAICHAPA BRENTFORD 4-1 NA KUJITANUA KILELENI


  TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa Darwin Nunez dakika ya 35, Alexis Mac Allister dakika ya 55, Mohamed Salah dakika ya 68 na Cody Gakpo dakika ya 86, wakati bao pekee la Brentford limefungwa na Ivan Toney dakika ya 75.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 57 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi mbili zaidi ya Arsenal baada ya wote kucheza mechi 25, wakati Brentford inabaki na pointi zake 25 mechi 24 nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA BRENTFORD 4-1 NA KUJITANUA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top