• HABARI MPYA

  Thursday, February 22, 2024

  ARSENAL WACHAPWA 1-0 NA PORTO LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, FC Porto wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Do Dragão mjini Porto.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji, Wenderson Galeno dakika ya 90 na ushei akimalizia kazi nzuri ya Mbrazil mwenzake, beki Otávio Ataide da Silva na timu hizo zitarudiana Machi 12 Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mechi nyingine ya jana 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya wenyeji, Napoli walitoa sare ya 1-1 na Barcelona, Robert Lewandowski akianza kuwafungia wageni dakika ya 60, Victor Osimhen kuwasawazishia wenyeji dakika ya 75 Uwanja wa Diego Armando Maradona Jijini Napoli.
  Nao watarudiana Machi 12 Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL WACHAPWA 1-0 NA PORTO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top