• HABARI MPYA

  Thursday, February 22, 2024

  AZAM FC YAWATANDIKA GREEN WARRIORS 5-0 ASFC CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Green Warriors leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mawinga, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 32, Muivory Coast Kipre Junior dakika ya 23, beki Paul Kyabo aliyejifunga dakika ya 56 na viungo washambuliaji, Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 65 na Ayoub Lyanga dakika ya 83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWATANDIKA GREEN WARRIORS 5-0 ASFC CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top