• HABARI MPYA

  Saturday, February 17, 2024

  SAKA APIGA MBILI ARSENAL YATANDIKA VIBONDE BURNLEY 5-0


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya wenyeji, Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Martin Odegaard dakika ya nne, Bukayo Saka mawili dakika ya 41 kwa penalti na 47, Leandro Trossard dakika ya 66 na Kai Havertz dakika ya 78.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 55, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Liverpool baada ya wote kucheza mechi 25, wakati Burnley inabaki na pointi zake 13 za mechi 25 nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKA APIGA MBILI ARSENAL YATANDIKA VIBONDE BURNLEY 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top